ELIMU YA KUJIUNGA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

  • Category: Kuhusu
  • Published: Friday, 24 November 2023 09:40
  • Written by bitta magesa rusweka
  • Hits: 367

Maana ya vyama vya wafanyakazi

1.Vyama vya wafanyakazi ni vyama ambavyo vimeanzishwa na wafanyakazi wenyewe kwa malengo ya pamoja ya kutetea na kudai maslahi yao na vyama vinaweza kuwa vya kisekta au  wafanyakazi mchanganyiko.

Ingawa vyama ambavyo vimeonekana kuwa na nguvu sana katika Nchi mbali mbali tangu kuanzishwa kwake ni vyama ambavyo vana muunganiko wa taaluma ambazo zinaendana kwa mfano Chama cha madaktari na wafamasia Tanzania ni chama ambacho wanachama wake ni madaktari na wafamasia wa ngazi zote za elimu na hata maslahi na haki zao zinafanana na zinakaribiana na hata mazingira yao ya kazi yanaendana tofauti na vyama ambavyo unakuta ni kama mfno wa kikapu cha sokoni unaweza kukuta kila aina ya taaluma ipo kwenye chama hii inakuw shida sana kufikia malengo kutokana na chama kuwa na watu ambao kuhalisia wanachama wake wana maslahi na changamoto zinazotofautaina.

2.Sheria ya ajira na mahusinao kazini namba 366/2019  katika kifungu cha  9 kinatoa haki kwa mfanyakazi kujiunga na chama,kuhudhuria mikutano ya chama bila kuingiliwa na mwajiri lakini kigezo kiwe kuwa mfanyakazi/mtumishi amafuata taratibu za kujiunga au kushiriki shughuli za chama cha wafanyakazi bila kuathiri shughuli zozote za mwajiri.

3.Nchini Tanzania kumekuwa na elimu duni sana inayohusu vyama vya wafanyakazi na hii imekuwa changamoto kubwa sana kwa wafanyakazi ambao wametamani kujiunga na vyama lakini hawana elimu ya kutosha kuhusu vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wengine wamejikuta wakiingizwa kwa vyama vya wafanyakazi ila ridhaa yao au baadhi ya maofisa wa waajiri mbali mbali kutumia udanganyifu au mamlaka walizonazo kuwaingiza/kuwachagulia vyama vya wafanyakazi bila ridhaa ya wafanyakazi wenyewe na malalamiko ya aina hii yamekuwa mengi sana kwa watumishi hasa wanapokuwa wanahitaji kutoka kwenye vyama ambavyo wameingizwa bila ridhaa zao.

4. Haki za chama na taratibu za kujiunga na chama

Kwa mujibu wa kanuni za sheria ya ajira na mahusino kazini  mfanyakazi anaweza kujiunga na chama kwa kutoa ridhaa yake mwenyewe kwa kujaza fomu ya kujiunga ambayo ni fomu namba TUF 15.

Baada ya kujaza fomu yake vizuri ataifikisha kwa mwajiri wake na nakala kwa chama chake

katika fomu ya kujiunga kuna kuwa na maelekezo ya kujiunga ambayo mfanyakazi ataweka taarifa zake kama zifuatazo

a.Jina la mtumishi.mfanyakazi

b.namba ya mfanyakazi au chek namba kwa waajiriwa wa Serikali

c.Jina la mwajiri  ambalo linaweza kuwa jina la taasisi au jina ambalo limesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Nchi  au kama ni mtu binafsi  jina lake

d.Jina la chama  mfanyakazi anachojiunga kama ni chama cha madaktari na wafamasia Tanzania ataandika

e.Ada ya chama kulingana na katiba ya chama chake kwa mfano chama cha wafanyakazi madaktari na wafamasia ni asilimia mbili  2%

swala la ada za vyama limekuwa linaleta changamoto kwa wafanyakazi wengi sana hasa wakitaka kujua nani anapanga ada za vyama vya wafanyakazi?

Kimsingi ada za vyama vya wafanyakazi zinapangwa na vyama vya wafanyakazi vyenyewe kisha kupeleka kwa msajili wa vyama vya wafanyakazi ili kupitishwa baada ya kuwa wanachama wamekubaliana na ada ya chama husika ingawa kutokana na ongezeko la vyama vya wafanyakazi Nchini kumekuwa na vyama ambavyo vinatoza 1% na vingine vikiwa na mfumo wa pesa taslimu.

Baada ya kujaza kulingana na maelekezo mfanyakazi ataweka jina sahihi na tarehe kwenye fomu na kuwa na shuhuda ambaye ataweka jina sahihi na tarehe kisha fomu itakuwa imekamilika nakuwasiishwa kwa mwajiri ili aweze kukata ada kwa mfano umechagua chama cha wafanyakazi madaktari na wafamasia Tanzania CODE YA CHAMA NI PC 7018 utaindika kwa juu ili mwajiri akuingize kwa makato  n atayari utakuwa umekuwa mwanachama

5.Makosa ya mazoea

Kumekuwa na makosa ya mazoea ambayo ufanywa na watu/viongozi wa taasisi kwa kujua au kutokujua kwa mfano kumkataza mtumishi/mfanyakazi kujiunga na chama au kumlazimisha kujiunga na chama au kumchagulia chama cha kujiunga  ni kosa kwa mujibu wa sheria ya kazi kifungu cha 102(3) na kuna uwezekano wa kupewa adhabu ya kulipa fidia ya shilingi milioni tano.

Ni muhimu kuacha watumishi/wafanyakazi kuwa huru na kuchagua vyama ambavyo wanaona wao wenyewe vitakuwa na manufaa kwao ili kufanya sehemu za kazi kuwa salama.

karibuni sana kwa mada zijazo za vyama vya wafanyakazi na waajiri

 

 

Mawasiliano

Tanzania Medical, Dental and Pharmaceutical Workers Union (TMDPWU) 
Post - Azikiwe/Jamhuri St Phoenix House 2nd Floor
P.O.Box 65498
+255 787 941 606 | +255 713 910 324  
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


Copyright © Tanzania Medical, Dental and Pharmaceutical Workers Union.. All Rights Reserved. Designed by microsafi.com