Falsafa ya chama
- Chama cha TMDPWU kinaamini kuwa afya ni haki na lazima ipatikane kwa gharama ambayo muhusika anaweza kuimudu, ipatikane kwa usawa kwa watu wote bila kujali cheo, rangi, kabila, dini, umbile, daraja la maisha wala umri naiweya uhakika na salama muda wote kwa wananchi wote wa Tanzania.
- Chama cha TMDPWU kinaamini kuwa afya ya watu wa Tanzania ina maanisha afya ya ujumla yaani ya kimaumbile, kiakili, kijamii, kiroho na kiuchumi na sikutokuwapokwaugonjwatu.
- Chama cha TMDPWU kinaamini kuwa maslahi bora ya wanachama wa TMDPWU na wafanyakazi wengine katika sekta ya afya ndiyo nyenzo muhimu katika utoaji wa huduma bora za afy akw aWatanzania wote.
