Uanachama wa Heshima

  • Category: Kuhusu
  • Published: Thursday, 17 August 2023 12:49
  • Written by Administrator
  • Hits: 347
Kutakuwa na uanachama wa heshima utakaotunukiwa mtu aliyetoa mchango wa pekee na uliotukuka katika kuendeleza mapambano ya wafanyakazi.
(a) Utaratibu wa kuteua mwanachama wa Heshima
{i} Kamati ya Utendaji ya Kanda itawasilisha jina la mhusika katika Kamati ya Utendaji ya
Taifa kwa uratibu kabla ya kupeleka kwenye Baraza Kuu
{ii}  Uteuzi  wa  uanachama  wa  Heshima  utafanywa  na  Mkutano  Mkuu  wa  chama kutokana na majina yaliyoratibiwa na kuwasilishwa kwake na Baraza Kuu.
(b) Wanachama wa heshima hawaruhusiwi kupiga kura kwenye mikutano yoyote ya Chama.
Michango ya Mwanachama
 
Michango ya Chama itakusanywa kutoka kwa wanachama kama ifuatavyo:
 
(a) Kiingilio cha unachama
 
{i} Mwombaji aliyekubaliwa uanachama atatakiwa kulipa kiingilio na kupewa kadi ya
Uanachama.
{ii}   Kima   cha   kiingilio  kitapangwa  na   Baraza   Kuu   na   malipo   yakishafanywa hayatarudishwa.
 
(b) Ada ya uanachama
 
Ada ya uanachama italipwa, kila mwezi kwa viwango vitakavyowekwa na Mkutano mkuu wa chama.
  1. 1. Utaratibu wa malipo ya ada za uanachama yatafanywa kama ifuatavyo:
{i} Ada ya uanachama italipwa moja kwa moja na mwajiri kwa kukatwa asilimia
2% katika mshahara na hii itawasilishwa kila mwezi kabla ya tarehe nane kwenye akaunti ya TMDPWU.
{ii} Kwa wale ambao hawatakuwa katika mfumo wa ajira kama kifungu 3.3(b)1{i} kinavyoelekeza, ada inaweza kulipwa na mwanachama mwenyewe tawini kwake na kupewa stakabadhi yake.
{iii} Ada zote za wanachama wa TMDPWU pamoja na ada ya uwakala zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa TMDPWU kila mwezi kabla ya tarehe kumi ya mwezi unaofuata.
  1. 2. Michango yoyote ya wanachama itapelekwa benki kwenye akaunti ya cha
  1. 3. Ruzuku za Kanda zitalipwa toka kwenye mfuko wa chama kwa viwango vitakavyopangwa na Baraza Kuu, ikizingatia uwiano wa wanachama ndani ya kanda husik
 
(c) Ada ya uwakala
 
Ada ya uwakala itakuwa sawa na kima cha ada ya uanachama na itakusanywa kila mwezi kutoka kwa wafanyakazi wasio wanachama.
 Kadi za Uanachama
 
Kila mwanachama atapewa kadi ya chama itakayobandikwa picha yake na kujazwa
 
(a) Jina lake
(b) Anuani yake
(c)  Kazi yake
(d) Tarehe ya kujiunga
(e) Maelezo mengine muhimu
 
3.5 Daftari la Kudumu
Kutakuwa na daftari la kudumu kwa madhaumuni yafuatayo
(a) Kuingiza maelezo yote  ya  mwanachama yaliyomo katika  kadi yake  na  kuhifadhi taarifa  zote  muhimu  zinazohusu  uhai  wa  mwanachama,  ikiwa  ni  pamoja  na michango aliyotoa.
(b) Ni wajibu wa viongozi wa ngazi zote za chama kutunza kumbukumbu zote muhimu zinazohusu uhai wa wanachama katika Daftari lake la kudumu.
 
 Mgawanyo wa ada za uanachama
 
(a) Makao  Makuu,  itarejesha  ruzuku  za  uendeshaji  katika  ngazi  za  Chama  kama ifuatavyo
{i}  Matawi  yatapelekewa  asilimia  ishirini  (20%)  ya   makusanyo  yao   (ambayo hayatokani na kukatwa mishahara moja kwa moja).
{ii}  Kanda zitapewa ruzuku na  Makao Makuu kwa  viwango  vitakavyopangwa na
Baraza Kuu kwa kuzingatia uwiano wa wanachama.
(b) Baada ya mwajiri kukata asilimia mbili (2%) ya ada ya uanachama atapeleka asilimia themanini 80% TMDPWU Makao Makuu na asilimia ishirini (20%) itabaki tawini.
 
Masharti na sifa za uanachama
(a) Awe na sifa zote zinazotajwa katika katiba ya chama
(b) Awe ni mwajiriwa mweye taaluma na kufanya kazi za udaktari au ufamasia
(c)  Awe na kadi ya uanachama
(d) Awe mwenye akili timamu
(e) Awe anayetimiza wajibu wake wa uanachama kwa vitendo
Haki za mwanachama
 
Mwanachama yeyote isipokuwa mwanachama wa heshima na shirikishi, atakuwa na haki zifuatavyo;
(a) Kuwakilishwa na Chama dhidi ya mwajiri wake au kujitetea yeye mwenyewe dhidi ya mwajiri huyo, akisimamiwa na chama, kwa kosa lolote linalohusu ajira.
(b) Kujitetea na kukata rufaa kwenye vyombo vya juu vya chama pale asiporidhika na uamuzi wa ngazi za chini.
(c)  Kushiriki katika chaguzi mbalimbali za chama
(d) Kuchagua viongozi na/au kugombea uongozi
(e) Kuhoji na kufahamishwa kuhusu mapato na matumizi ya mali na fedha za Chama.
(f)  Kuwa  mdau  wa  mambo  yote  yanayokihusu chama  ikiwemo  rasilimali  na  vitega uchumi.
 
Wajibu wa Mwanachama
Kila mwanachama, isipokuwa wanachama wa heshima na shirikishi atakuwa na wajibu wa
 
(a) Kulipa  ada  ya  kila  mwezi  na  malipo  maalumu  na  kuhakikisha  imewasilishwa panapohusika kwa wakati unaotakiwa.
(b) Kuunga mkono na kusaidia kwa vitendo maendeleo ya chama
(c)  Kuzingatia Katiba, kanuni na taratibu za chama na kuheshimu maamuzi yaliyotokana na kanuni au taratibu hizo.
(d) Kushiriki katika shughuli zote za chama na mikutano.
Miiko ya mwanachama
 
(a) Mwanachama  wa  TMDPWU  hatajihusisha  au  kushiriki  katika  vikao  au  mikutano inayojadili hoja za kupingana na Katiba, Kanuni, au Miongozo ya Chama.
(b) Hatashiriki katika migomo au maandamano au hatua nyingine zozote zile za ushinikizaji ambazo hazikuandaliwa au kukubalika na Chama.
(c)  Hatatoa lugha chafu ya matusi kwa viongozi wa Chama, mwajiri au kwa wanachama wenzake.
(d) Hatatoa kauli za uongo zinazohusu Chama mahali popote pale
 
Kukoma Uanachama
 
(a) Mwanachama atakoma kuwa mwanachama iwapo
  1. 1. Hatawasilisha michango yake kwa miezi mitatu mfululizo kwa makusudi
  1. 2. Atajiuzulu uanachama kwa kuiandikia Halmashauri ya Tawi lake juu ya uamuzi wake
  1. 3. Atafariki
  1. 4. Atafukuzwa uanachama kwa mujibu wa kifungu 3.13
  1. 5. Atafungwa jela kwa kosa la jinai
  1. 6. Ataugua ugonjwa wa akili na kushindwa kuzingatia kanuni, taratibu na katiba ya
Chama.
(b) Mwanachama ambaye uanachama wake umekoma ataitaarifu Halmashauri ya Tawi lake ambayo italiondoa jina lake kwenye orodha ya wanachama nakurudisha kadi ya Chama.
(c)Mtu yeyote ambaye uanachama wake umekoma hatakuwa na haki wala wajibu wowote katika chama.
Kufukuzwa Uanachama
 
(a)Mwanachama  yeyote  anaweza  kufukuzwa  katika  chama  iwapo   mamlaka  husika itathibitisha kwamba:
  1. 1. Amejipatia uanachama kwa njia ya udanganyifu
  1. 2. Amekosa uaminifu, amefuja na/au kupoteza mali na fedha za chama
  1. 3. Ana uanachama wa chama kingine cha wafanyakazi
  1. 4. Amefanya vitendo vinavyopinga katiba au maamuzi ya Mkutano Mkuu
  1. 5. Amekosa uzalendo, utii na amekisaliti Chama katika migogoro ya kikazi
(b) Utaratibu wa kumfukuza mwanachama utakuwa kama ufuatao:
  1. 1.Halmashauri ya Tawi, baada ya majadiliano na mwanachama mtuhumiwa, itatoa maelezo ya maandishi kwa Kamati ya utendaji ya Kanda ikipendekeza adhabu/hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiw
  1. 2. Kamati ya utendaji ya Kanda itajadili tuhuma dhidi ya mwan achama mhusika na ikiamua kumfukuza uanachama itapeleka taarifa ya maandishi kwa Kamati ya Utendaji ya Taifa ikipendekeza kufukuzwa uanachama mtuhumiwa huyo.
  1. 3. Kamati ya Utendaji ya Taifa itazipitia tuhuma zilizopelekewa na ikiyakubali mapendekezo yaliyotolewa na Kanda, itawasilisha mbele ya Baraza kuu jina la mwanachama mtuhumiwa, kwa uamuzi wa mwisho.
Mwanachama anayependekezwa kufukuzwa kwenye chama, anayo haki ya kujulishwa tuhuma zinazomkabili; kukata rufaa, kutoa na kusikilizwa utetezi wake katika ngazi zote husika hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa.
 
Kuhamia katika Tawi jingine la Chama
Mwanachama anayehama sehemu moja ya kazi kwenda sehemu nyingine katika moja ya kazi za taaluma ya udaktari na ufamasia, atatoa taarifa hizo katika Tawi mahali au sehemu hiyo au lililo karibu na hapo na hivyo kuweza kuendelea kuwa mwanachama halali.
 
Kuhamia TMDPWU kutoka Chama kingine
Mwanachama wa Chama kingine cha wafanyakazi mwenye sifa za kujiunga na TMDPWU anaweza kuhamia TMDPWU baada yakubatilisha uanachama wake wa Chama chake cha awali kwa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa mwajiri na Chama anachohama kwa mujibu wa sheria Na.366 ya Ajira na Mahusiano kazini ya 2019.

Mawasiliano

Tanzania Medical, Dental and Pharmaceutical Workers Union (TMDPWU) 
Post - Azikiwe/Jamhuri St Phoenix House 2nd Floor
P.O.Box 65498
+255 787 941 606 | +255 713 910 324  
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


Copyright © Tanzania Medical, Dental and Pharmaceutical Workers Union.. All Rights Reserved. Designed by microsafi.com