Uwanachama
Maombi ya kujiunga na Chama yataambatana na ujazaji wa fomu ya makato ya ada za Chama iliyoelekezwa (TUF 15 ) kama ilivyoanishwa katika Sheria Na. 366 ya Aira na Mahusiano kazini ya
2019 kifungu cha 61. Chama cha TMDPWU kitakuwa na aina mbili za wanachama;
Wanachama wa Kawaida
(a) Wanachama waanzilishi
Wanachama wote watakaokuwa kwenye orodha kabla ya kuanzishwa kwa Chama na watakamilisha taratibu za kujiunga na Chama hiki baada ya kuanzishwa watahesabiwa kuwa waanzilishi wa Chama cha TMDPWU. Mwanachama mwanzilishi atakuwa na haki na wajibu kama mwanachama mwingine yeyote wa TMDPWU.
(b) Wanachama Wapya
Maombi ya uanachama
Utaratibu wa kupata wanachama wapya au wengine, mbali na waanzilishi ni:
Maombi ya kutaka uanachama yatapelekwa kwenye halmashauri ya Tawi ya mahali anapofanyia kazi mwombaji. Pale ambapo hapana tawi maombi yatapelekwa katika ofisi ya Chama iliyo karibu.